Thursday, January 28, 2016

ACT WATOA KAULI NZITO KWA RAIS MAGUFULI.

JANA limetokea tukio la aibu katika nchi yetu pale serikali ilipofanya jaribio la hatari la kuzuia wananchi kuona na kusikia kinachoendelea bungeni.

Kitendo cha serikali ya CCM kuzuia kuonyeshwa moja kwa moja vipindi vya bunge katika televisheni ya taifa ni cha kijima na sisi chama cha ACT-Wazalendo tunakilaani kwa nguvu zetu zote.
 
Tunakitafsiri kitendo hiki cha serikali kama mwendelezo wa hatua na juhudi za Rais Magufuli za kuminya demokrasia na kusimika utawala wa kiimla.

Tunawasihi wananchi kusimama imara na kuzipinga jitihada zozote ovu za kuminya demokrasia nchini.
 
Tunawapongeza wabunge wazalendo wa upinzani kwa kusimama pamoja na kupinga nia ovu ya serikali ya kuua demokrasia katika nchi yetu.

Tunawatia shime wabunge wote wazalendo kuendelea kupigania maslahi mapana ya taifa letu.

ACT-Wazalendo! Taifa kwanza leo na kesho!

Imetolewa na;
Samson Mwigamba,
KATIBU MKUU.

Magazeti ya Leo Ijumaa



Tuesday, January 26, 2016

Le Mutuz Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu Amvaa Benard Membe.

Lemutuz
Kufuatia kauli za aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa katika awamu ya nne Bernald Membe, kuonekana kupinga juhudi za Rais John Pombe Magufuli kwenye masuala mbalimbali ikiwemo suala la Safari za nje kwa viongozi wa Umma.lemutuzzzzsss

Mtoto wa aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania John Malecela, anaefahamika kwa jina la Le Mutuz Nation amefunguka ya moyoni na kueleza kuwa anachokifanya Membe sio ustarabu kwa serikali ya Magufuli kwani hajatumia ustarabu kama kiongozi na kuamua kuonesha ubinafsi.

Ameandika Kama Ifuatavyo;

LIVE STRAIGHT TALK:- MORNING GUYS MEMBE AMETUKOSEA SANA WATANZANIA KWA KAULI ZAKE KALI ZA KUKEMEA JUHUDI ZA MABADILIKO YA RAIS MAGUFULI AMBAYE NDIO KWANZA ANAKARIBIA KUTIMIZA MWEZI WA PILI KATIKA MADARAKA INFACT MEMBE AMEONYESHA TABIA MOJA ISIYOKUWA NZURI SANA KWETU WOTE BINADAM YAANI UBINAFSI AU SELFISHNESS…I MEAN RAIS MAGUFULI ANACHOKIFANYA NI KILE ALICHOKIAHIDI AMBACHO HATA MEMBE MWENYEWE ALIKIUNGA SANA MKONO KWENYE KAMPENI ZA URAIS NA SISI WOTE MAGUFULI ALISEMA WAZI KWAMBA TAIFA LIMEOZA MEMBE ALIKUWA NA NAFASI KUBWA KUMKATALIA THEN KWAMBA SIO KWELI TAIFA HALIJAOZA KWA SABABU LABDA MOJA YA SABABU YA MEMBE KUJITOKEZA NOW NA KAULI KALI NI KUJARIBU KUTETEA RECORD YA UTAWALA ALIOKUWA MSHIRIKI WA KARIBU NA RAIS ALIYEPITA BASI ANAKOSEA SANA KWA SABABU TULIMKATAA LOWASAA KWA KUWA ALIKUWA RAFIKI NA MATAJIRI NA WALIOTUAMBIA KWAMBA LOWASSA HAFAI NI PAMOJA NA YEYE MWENYEWE MEMBE SASA LEO KWELI TENA MEMBE ANASIMAMA KUSHAMBULIA KAZI ZA MAGUFULI KWA NIABA YA WAFANYABIASHARA? ….PLEASE MEMBE ATUOMBE RADHI WATANZANIA MILLIONI 50 TULIOMCHAGUA MAGUFULI CAUSE SISI BADO HATUJALALAMIKA KIVILEEE KAMA YEYE MTU MMOJA AMBAYE HAPA ANAKUWA KIGEU GEU NI YEYE MEMBE ALIYESIFIA UAMUZI WA MAGUFULI KUSIMAMISHA SAFARI ZA NJE KWA MAOFISA WA SERIKALI AKASEMA “TULIKUWA TUNAPISHANA JUU KWA JUU KAMA NYUMBANI KUNA MOTO” LEO MWEZI MMOJA NA NUSU LATER MEMBE TENA AMEBADILIKA ANASEMA SAFARI NI LAZIMA? WHY? …..JANA NILIKUWA MSTAARABU KIDOGO NILIDHANI MEMBE ALIPITIWA TU LAKINI KUMSIKIA AKIZUNGUMZA TENA JANA NASEMA HAPANA AGENDA ALIYONAYO MEMBE THIS TIME AROUND SIO YETU WANANCHI NINAANZA KUWA NA WASI WASI LABDA RAIS JK ALIWAPA WATU WENGI VYEO KWA USHAURI WA MEMBE NDIO MAANA SASA ANAUMIA KUONA ALIKUWA ANAMSHAURI VIBAYA RAIS LIKE SIO SIRI MKURUGENZI WA NIDA ALIKUWA NI RAFIKI WA KARIBU SANA WA MEMBE JANA TU IMEDHIRIKA HUENDA AMEFUJA KARIBU TSH. 156 BILLION ZA KODI ZETU KWENYE VITAMBULISHO VYA TAIFA NOW NIAMBIE KIPI CHA AJABU MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UMMA AMEPATA WAPI MAPESA YA AJABU MPAKA KUJENGA MRC PALE NYUMA YA SHOPPERS PLAZA MIKOCHEN? …I MEAN KUNA MAMBO MENGINE WANATUFANYA KAMA WATOTO WHY? MEMBE AMEZUNGUMZA KUTETEA WAFANYABIASHARA NA MEDIOCRE LEADERS IT IS WRONG ATUOMBE RADHI WANANCHI! – LE MUTUZ

Rukwa farmers shocked by 'foreign' tomato disease.

 Image result for tomatoes photo
 FARMERS in Nkasi District, Rukwa Region have expressed their fears on the invasion of a dangerous tomato disease known as ‘Tuta Absoluta’, which was for the first time brought into the country in 2014.
 
For the past one year since the tomato disease was reported in the country, it was only found in the three regions of Arusha, Kilimanjaro and Morogoro.
The Southern Highlands zone, which comprises Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma and Rukwa regions, was free from the disease.
 
According to Nkasi District Agricultural Officer, Henry Sing'ombe, the disease is linked with ‘Tuta Absoluta’—a devastating tomato pest, which originated from South America. 
 
‘Tuta Absoluta’ sucks water from the plant through tomato leaves. The leaves are left with pathogen, which circulate throughout the plant ending up with dried leaves, stem and roots.
 
The official said the disease which was reported to have hit the area in December last year; attacks tomato leaves and thereafter affects the entire growth of the plant.
 
“When studied, we discovered that it’s ‘Tuta Absoluta’ and we started putting in place strategies to arrest the dangerous tomato miner.
 
“The strategies include applying pesticides such as March 500 EC, Actra 25 EC and Buffalo100 EC. We managed to reduce the scale of the disease, but we’ve a lot to do to phase-out the disease,” Sing’ombe said.
 
He added that mixtures of Evisect 50 SP, Escotin 0.15 EC, Covagen 5C and Belt 480 5C, which are very expensive, are also used to contain the disease.
 
“Other strategies include educating farmers on how to tackle the disease; as well as informing them on the need for them to leave farms affected with the disease for a while.”
 
The official said his office has contacted the Agricultural Research Institute - Uyole (ARI-Uyole), so that they come up with long-lasting solutions to the disease.
 
Nkasi District-based farmer Boniface Msafiri said he was afraid that he will not harvest anything in his farm because of the disease.
 
He said that the disease is very challenging and immediate efforts from different players in the agriculture sector are needed.
 
Flora Mwaga, who is a small-scale tomato grower in Sumbawanga District, complaining on the new disease, called upon the government to chip-in and assist them on how to do away with the disease.
 
She also urged extension officers to visit farmers in their farming fields to see how big the scale of the problem is.
 
The Tomato miner ‘Tuta absoluta’ was reported in Tanzania for the first time in August 2014 in Arumeru District, Arusha Region.
 
Recently, ‘Tuta Absoluta’ was considered to be a serious threat to tomato production in the Mediterranean region. The newly imported pest from South America finds the shores of the Mediterranean a perfect new home where it can breed between 10 and 12 generations a year. 
 
Each female can lay 250-300 eggs in her life time.  The pest is crossing boarders and is destroying tomato production both protected and in open fields.

Monday, January 25, 2016

Mama Amuua Mwanae Kwa Kichapo.


Mtoto wa miaka 11, Nchambi Tungu, ameuawa kikatili na mama yake mzazi kwa kuchapwa fimbo kisha kumfunga kamba shingoni na kumning’iniza kwenye tawi la mwembe ili ionekane kuwa amejinyonga mwenyewe.

Inaelezwa kuwa mama wa mtoto huyo, Sado Roketi (26) mkazi wa kitongoji cha Mnyakasi, kijijini Ikuba, wilayani Mlele, mkoa wa Katavi alimuua mwanawe huyo baada ya kukataa kumfulia nguo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, jana alithibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Alisema tukio hilo ni la Januari 23, mwaka huu saa moja jioni katika Kitongoji cha Mnyakasi. Alisema siku ya tukio mtuhumiwa alimpatia mwanawe huyo nguo amfulie lakini mtoto huyo alikataa kuzifua akaendelea kucheza na wenzake.

“Ndipo mama huyo kwa hasira alipoamua kuchukua fimbo na kuanza kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia kifo, aliubeba mwili na kuutundika kwenye matawi ya mti wa mwembe baada ya kumfunga kamba shingoni na kumwacha akining`inia ili ionekane alijinyonga mwenyewe,” alieleza Kidavashari .

Alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Friday, January 22, 2016

HII NDIO SHUGHULI YA WANCHI WA MKOA WA SONGWE NA MAZINGIRA.


WanaTAJATI pia walipata fursa ya kushiriki upandaji wa miti kuzunguka eneo la Hospitali ambapo miti zaidi ya 50 ilipandwa


Mbali na kupanda miti pia walifanya usafi katika mazingira yanayoizunguka Hospitali ya Wilaya ya Chunya

TAJATI wakishiriki ujenzi wa daraja kubwa lililojengwa kwa nguvu za wananchi wa Kijiji cha Igangwe kata ya Mtanila Wilaya ya Chunya linaloviunganisha vitongoji vya Shauri Moyo na Mtukula

Mwenyekiti wa TAJATI Ulimboka Mwakilili akishirikiana na Mwenyekiti wa Igangwe Amcos kuzindua zoezi la upandaji wa miti katika Shamba la Chama cha Msingi cha Igangwe ambapo miti zaidi ya 1000 ilipandwa

Wakulima wa Igangwe amcos wakishirikiana na Wanachama wa TAJATI katika upandaji wa miti

Makamu Mwenyekiti wa TAJATI, Christopher Nyenyembe akikagua timu za mpira wa miguu kabla ya kuanza kwa mtanange katika kuadhimisha mapinduzi ya Zanzibar


Mtunza Hazina wa TAJATI, Brandy Nelson akimkabidhi zawadi nahodha wa timu ya msindi wa Kwanza katika mechi maalum ya kuenzi mapinduzi ya Zanzibar

Katibu Mkuu wa TAJATI, Venance Matinya, akimkabidhi zawadi ya mpira wa miguu nahodha kwa niaba ya timu yake baada ya kuibuka kidedea katika shindano maalum la kuenzi mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika Lupa wilayani Chunya

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Sophia Kumbuli akiwa katika kikao cha majumuisho ya ziara ya waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI).

Makamu Mwenyekiti wa TAJATI akiagana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
 
 
BAADHI ya Wanachama wa Chama  cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) walifanya ziara ya siku tatu katika Wilaya ya Chunya na kushiriki shughuli mbali mbali za kijamii na kihabari.
 
Waandishi hao walifanya ziara hiyo jumatatu na kukamilisha jumatano ya wiki hili ambapo wakiwa Wilayani Chunya walipokea taarifa ya hali ya utalii ya Wilaya ya Chunya na kushiki shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
 
Akizungumza katika majumuisho ya Ziara hiyo iliyojumuisha waandishi 12, mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Sophia Kumbuli, Mwenyekiti wa TAJATI, Ulimboka Mwakilili alisema katika ziara hiyo iliyokuwa na mafanikio imepokelewa vizuri na wananchi.
 
Alisema siku ya kwanza waandishi waliweza kutembelea wagonjwa na kutoa zawadi kidogo ikiwemo sabuni za kufulia na vinywaji aina ya Grandmalt kwa ajili ya kuongeza nguvu sambamba na usafi wa mazingira ulioenda sambamba na uzinduzi wa kupanda miti ambapo miti zaidi ya 50 ilipandwa kati ya 560 inayotarajiwa kupandwa na Hospitali hiyo.
 
Aliongeza kuwa siku ya pili waandishi hao walishiriki katika ujenzi wa daraja la Mto Lupa katika Mto kijiji cha Igangwe linalounganisha Kijiji hicho na Vitongoji wa Shauri Moyo na Mtukula lenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni Mbili.
 
Aliongeza kuwa baada ya kushiriki ujenzi wa daraja hilo waandishi hao pia walijumuika na wakulima wa Chama cha Msingi cha Igangwe Amcos katika zoezi la upandaji wa miti ambapo zaidi ya miti laki moja ilipandwa ikiwa ni kutekeleza utunzaji wa mazingira na kampeni ya kata mti  panda miti.
 
Zoezi hilo la upandaji miti limetokana na wakulima wa Tumbaku kutumia miti kwa kiasi kikubwa wakati wa kuandaa zao la Tumbaku hadi mavuno jambo lililopelekea uongozi wa Amcos kuweka sheria na kanuni kwa kila mkulima kuhakikisha anapanda miti 500 katika shamba la Chama cha msingi na 25 shambani kwake.
 
Mwakilili alisema mbali na kushiriki shughuli hizo pia waandishi walizungumza na wananchi kuhusu changamoto zinazowakabili ambapo mambo mengi yalibainishwa ikiwemo ndoa za utotoni, mimba mashuleni na upungufu wa wahudumu wa afya katika kituo cha Afya Mtanila ambacho kina watumishi wanne tu.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Sophia Kumbuli mbali na kuwapongeza WanaTAJATI  kwa ziara yao pamoja na shughuli zingine za kimaendeleo na kijamii aliahidi kuyafanyia kazi mapungufu yaliyobainishwa.
 
Kuhusu ndoa za utotoni Mkurugenzi alisema atawasiliana na Kamati ya Ulinzi na uasalama ya Wilaya ili kuanza utekelezaji wa kuwasaka wanaume wanaooa mabinti wadogo na kuwakatika katika masomo yao.
 
Alisema suala la afya kutokuwa na watumishi wa kutosha alisemahilo ni tatizo la Wilaya nzima ingawa Serikali inatarajia kutangaza nafasi za kuajiri hivyo tatizo hilo linaweza kupungua kwa kiasi Fulani.
 
“Niwapongeze kwa juhudi zenu na ninawaahidi kuyafanyia kazi mambo yote mliyoyabaini mkiwa Wilayani Chunya hususani suala la kuozesha watoto wadogo hili limenisikitisha mno na sitalifumbia macho nitatoa taarifa kwa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ili wahusika wasakwe mara moja huu ni ukatili wa kijinsia” alisisitiza Mkurugenzi.

Thursday, January 21, 2016

NECTA YATANGAZA MATOKEO YA DARASA LA IV

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya mitihani ya kujipima ya darasa la nne huku matokeo hayo yakionyesha wanafunzi wengi wamefeli katika somo la Kiingereza kwa asilimia 65.67 katika mitihani hiyo iliyofanyika mwishoni 2015.

Akitangaza matokeo hayo leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde amesema juhudi za makusudi zinahitajika katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzia ili kuboresha kiwango cha ufaulu.

Jumla ya wanafunzi 869,057 kati ya wanafunzi 977,886 sawa na asilimia 88.87 waliofanya upimaji wamepata alama katika madaraja ya A,B,C,na D. Wanafunzi 108,829 sawa na asilimia11.13 wamepata alama za ufaulu usioridhisha.
Aidha wanafunzi wamefanya vizuri zaidi katika somo la Sayansi kwa asilimia 89.44, na baraza limewataka walimu kuweka mkazo zaidi kwa wanafunzi waliofanya vibaya ili wafanye vizuri.

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

SFNA-2015 ASSESSMENT RESULTS




NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA SFNA-2015 ASSESSMENT RESULTS

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

SFNA-2015 ASSESSMENT RESULTS



Education stakeholders want infrastructure shortage in primary schools addressed.

EDUCATION stakeholders have called on the government to take immediate action to address the shortage of infrastructures in primary schools as a way of improving the quality of free-education across the country.
 
The actors have it that while the government was very ambitious in offering ‘subsidised’ education from primary to lower secondary level, it was a concern that most schools face acute shortage of learning facilities.
 
Simon Kulian, a lecturer with Bagamoyo based Adem Institute said most schools recorded a high turnout of pupils who registered for primary education, unfortunately there are no sufficient classrooms to accommodate them. 
 
Speaking at a consultative meeting with headteachers from eight primary schools in Kinondoni and Temeke municipalilites, the education expert said the government initiative was a milestone for the sectors’ development. 
 
“We’re here for a consultative workshop. The meeting is designed to impact leadership skills to headteachers to effectively participate in classroom activities and thus improve the sector’s performance,” he said. The workshop was organised by Organisation for Community Development (OCODE).
He explained that while the government had made it clear, as stakeholders “we’re also playing our part to ensure that the sector is made better for the new generation.” 
 
Florida Nfura, headteacher of Buza Primary School in Temeke Municipality told reporters yesterday that her school had registered 730 pupils this year and it’s number is likely to increase. 
 
She said the number was twice higher than the 360 pupils registered in the last academic year. According to the headteacher, the new registration shows that the general public wants children access their fundamental right for education. 
 
“This has pushed us to allocate at least five classrooms of between 130 and 140 pupils,” she said, noting that earlier she made some arrangements that is why it has been possible to accommodate all the pupils and neither of them sits on the floor. 
 
Martha Kusenga, Kinondoni Municipal Education Officer told reporters in Dar es Salaam yesterday that the council has already started assessment to identify areas with acute shortage of classrooms for urgent support. 
She said registration of pupils will end in March 31, this year and that in a meantime preliminary findings indicate that this year there will be more enrollment of pupils. 
 
“Our daunting challenge is the ongoing demolition. Pupils are being transferred and you may find out that some places have been overwhelmed while others have less numbers of registered pupils.” 
 
OCODE Programme Doreen Matekele said they are now implementing a three-year programme in collaboration with an international NGO -- WE World to help improve the quality of education in primary schools in the two municipalities. 
 
“We’re training teachers, inspectors and education officers,” she said naming the benefiting schools as Buza, Bwawani, Kibonde Maji, Mtoni Kijichi, Kawe A, Bunju A, Mtambani and Tumaini.

Jotoardhi ni muhimu kwa Tanzania: Kamishna wa Nishati

Kutokana na ongezeko la mahitaji ya nishati ya umeme nchini, nishati itokanayo na jotoardhi imeelezwa kuwa muhimu kwa kuwa itachangia katika kukidhi mahitaji ya nishati   ambayo ni kiunganishi kikuu cha ukuaji wa uchumi.
Akiwasilisha mada katika Kongamano la Tano la Kimataifa la Jotoardhi kwa nchi za Bonde la Ufa, lililofanyika jijini Arusha kuanzia tarehe 27Oktoba – 2 Novemba, 2014, amesema kuwa jotoardhi inaweza kuwa suluhisho la mahitaji ya nishati kwa Tanzania na dunia.
Kamishna wa Nishati na Petroli Eng. Hosea Mbise akifafanua jambo
Kamishna wa Nishati na Petroli Eng. Hosea Mbise akifafanua jambo
“Tanzania inahitaji nishati mchanganyiko ikiwemo itokanayo na jotoardhi ili kukidhi mahitaji ya nishati ya umeme nchini ambayo mahitaji yake yamekua kwa kiasi cha asilimia 12-15 kwa mwaka mmoja,” alieleza Mhandisi Mbise.
Kamishna Mbise alifafanua kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2015 Tanzania itakuwa imeunganishwa na nishati ya umeme unaofikia kiasi cha megawati 3000 ambapo ifikapo mwaka 2033 kiasi cha megawati za umeme 10,000 zinatarajiwa kuzalishwa.
Alieleza kuwa, zipo fursa kwa sekta binafsi kushiriki katika shughuli za uwekezaji na uendelezaji wa nishati hiyo kutokana na uwepo wa Sera mpya ya Nishati ya mwaka 2014 ambayo imezingatia masuala ya nishati jadidifu ikiwemo jotoardhi, Sheria ya umeme ya mwaka 2008, Sera ya ushiriki wa sekta ya Umma na Sekta Binafsi ya mwaka 2009 na taratibu nyinginezo.
Kamishna Mbise alisema kuwa, Serikali itahakikisha kuwa inaendeleza nishati ya jotoardhi kutokana na mazingira bora yanayoruhusu kuendeleza nishati hiyo ikiwemo kuanzishwa kwa Kampuni ya Maendeleo ya Jotoardhi ya Taifa (TGDC), mchango wa serikali katika kusaidia masuala ya uchorongaji katika maeneo ya Ziwa Ngozi na Songwe Mkoani Mbeya, katika Ziwa Natron (Manyara), Kisaki Morogoro na Luhoi (Pwani).
Aidha, Kamishna Mbise alisema kuwa, taasisi za Kimataifa zimetoa kipaumbele cha kuendeleza jotoardhi Tanzania na Afrika zikiwemo Benki ya Dunia (WB), Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB), Shirika la Umoja wa Maendeleo la Japani (JICA), Shirika la Kimataifa linaloshughulikia Mazingira (UNEP) na Shirika la Misaada la Watu wa Marekani (USAID). Ameongeza kuwa ushirikiano huo na mazingira wezeshi yataiwezesha Tanzania kufikia lengo la kuzalisha megawati 200 zitakazotokana na jotoardhi ifikapo mwaka, 2020.
Imeandaliwa na:
Asteria Muhozya,
Afisa Habari,
Wizara ya Nishati na Madini,
754/33 Mtaa wa Samora,
S.L.P 2000 Dar es Salaam,
Simu: +255-22-2121606/7, Nukushi: +255-22-2121606
Barua Pepe: info@mem.go.tz
Tovuti: www.mem.go.tz

UBA TANZANIA TRAINS IFM (INSTITUTE OF FINANCE MANAGEMENT) STUDENTS ON CUSTOMER SERVICE MANAGEMENT‏

Kwa wanavyuo wote watanzania popote Duniani Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. Tumieni mtandao huu ni wenu nyote. 
uba 1
Service Quality Manager, Queen Odunga during the training session at IFM (Institute of Finance Management).

uba 2
Some of the students present at the training take a group picture with UBA staff members.
uba 3
A student ask a question during the training session with UBA Team on customer service management.
uba 4
Some of the students present at the training take a group picture with UBA staff members.
uba 5
Some of the students present at the training.
Saturday, 16 January 2016 UBA trained IFM students on customer service management. Taking on the session was the Service Quality Manager, Queen Odunga, who explained how to handle a difficult customer. And after the session, the students tried to create a situation where the customer is complaining and doesn’t want to listen to the CSO. This came out so well as the one who was acting as CSO resolved the situation and the one acting as the client was happy that his problem was solved.
One happy student commended the UBA Team for taking them through the session “This has been a great session that we cannot easily get from our daily lectures. We thank UBA team especially Madam Queen who has highlighted on the importance and tactics of how to handle a difficult customer”, She concluded.
Queen Odunga the Service Quality Manager thanked the IFM Management for giving UBA the platform to share the knowledge on Customer service. She also applauded the students being attentive. “I would like to thank the IFM Management for providing UBA Tanzania with this platform and I would also like to thank the students for attending in numbers and being attentive throughout the session, it was quite interactive”. She continued by advising the students to take heed of the knowledge they have achieved in this session as “customer service is very vital for any business as it leads to customer retention and business development”.
Other UBA team members present at the session were also able to interact with the students giving them advise on the dos and don’ts in the finance and banking industry at large.

Mkuu wa Oganaizesheni wa NCCR-Mageuzi Amtaka LOWASSA Ajieleze Kama Ataendelea Kubaki CHADEMA Iwapo Jina lake Litaenguliwa Mbio za Urais 2020


Kufuatia  kauli ya aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwavuli wa Ukawa, Edward Lowassa ya kugombea tena urais mwaka 2020, Mkuu wa Oganaizesheni wa NCCR-Mageuzi, Faustine Sungura amemhoji Lowassa kama atakuwa tayari kuendelea kutumikia Ukawa kama jina lake halitapendekezwa kugombea nafasi hiyo.
Sungura amesema kauli hiyo ya Lowassa kupambana tena katika kinyang’anyiro cha urais mwaka 2020 kunategemea maamuzi ya chama kupitisha jina lake.

“Nimemsikia Lowassa anasema kuwa anajiandaa kupambana na Rais John Magufuli mwaka 2020, lakini je, yuko tayari kuheshimu maamuzi ya chama kwa maslahi ya wakati huo?” Alihoji Sungura.

Sungura alisema mwaka jana jina la Lowassa lilipochujwa kwenye wagombea urais ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alijiondoa na kuhamia Chadema.

“Je, atakuwa tayari kuheshimu maamuzi ya chama pale ambapo jina lake halitapitishwa kugombea urais Chadema au atahamia chama chake?” Alihoji Sungura.

Akizungumzia ushindi wa viti vya meya uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita, Sungura alisema ushindi huo ambao wameshinda wagombea wa Chadema na CUF usitafsiriwe kuwa ni ushindi wa Ukawa, bali ni ushindi wa Chadema na CUF .

“Nasema hayo kwa sababu ukizungumzia Ukawa unazungumzia vyama vinne ambavyo ni Chadema, NCCR Mageuzi, NLD na CUF, lakini kilichofanyika kuna baadhi ya kata tulisimamisha wagombea lakini walituwekea kauzibe tusipate,” alisema Sungura.

Sungura alisema baadhi ya vyama ndani ya Ukawa wana ubinafsi kuwachanganya watanzania kwa neno Ukawa ambalo halina maana yoyote badala yake kuviua vyama vingine ndani ya umoja huo.

MKOANI SONGWE

MKOANI SONGWE PICHA YAKE KWA MBELE
MKOA WA SONGWE VIBAO VYA MATANGAZO
BARABARA YA KIMATAIFA
PICHA YA MIGOMBA KWA MBALI