Thursday, January 28, 2016

ACT WATOA KAULI NZITO KWA RAIS MAGUFULI.

JANA limetokea tukio la aibu katika nchi yetu pale serikali ilipofanya jaribio la hatari la kuzuia wananchi kuona na kusikia kinachoendelea bungeni.

Kitendo cha serikali ya CCM kuzuia kuonyeshwa moja kwa moja vipindi vya bunge katika televisheni ya taifa ni cha kijima na sisi chama cha ACT-Wazalendo tunakilaani kwa nguvu zetu zote.
 
Tunakitafsiri kitendo hiki cha serikali kama mwendelezo wa hatua na juhudi za Rais Magufuli za kuminya demokrasia na kusimika utawala wa kiimla.

Tunawasihi wananchi kusimama imara na kuzipinga jitihada zozote ovu za kuminya demokrasia nchini.
 
Tunawapongeza wabunge wazalendo wa upinzani kwa kusimama pamoja na kupinga nia ovu ya serikali ya kuua demokrasia katika nchi yetu.

Tunawatia shime wabunge wote wazalendo kuendelea kupigania maslahi mapana ya taifa letu.

ACT-Wazalendo! Taifa kwanza leo na kesho!

Imetolewa na;
Samson Mwigamba,
KATIBU MKUU.

Magazeti ya Leo Ijumaa



Tuesday, January 26, 2016

Le Mutuz Mtoto wa Waziri Mkuu Mstaafu Amvaa Benard Membe.

Lemutuz
Kufuatia kauli za aliyekuwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa katika awamu ya nne Bernald Membe, kuonekana kupinga juhudi za Rais John Pombe Magufuli kwenye masuala mbalimbali ikiwemo suala la Safari za nje kwa viongozi wa Umma.lemutuzzzzsss

Mtoto wa aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania John Malecela, anaefahamika kwa jina la Le Mutuz Nation amefunguka ya moyoni na kueleza kuwa anachokifanya Membe sio ustarabu kwa serikali ya Magufuli kwani hajatumia ustarabu kama kiongozi na kuamua kuonesha ubinafsi.

Ameandika Kama Ifuatavyo;

LIVE STRAIGHT TALK:- MORNING GUYS MEMBE AMETUKOSEA SANA WATANZANIA KWA KAULI ZAKE KALI ZA KUKEMEA JUHUDI ZA MABADILIKO YA RAIS MAGUFULI AMBAYE NDIO KWANZA ANAKARIBIA KUTIMIZA MWEZI WA PILI KATIKA MADARAKA INFACT MEMBE AMEONYESHA TABIA MOJA ISIYOKUWA NZURI SANA KWETU WOTE BINADAM YAANI UBINAFSI AU SELFISHNESS…I MEAN RAIS MAGUFULI ANACHOKIFANYA NI KILE ALICHOKIAHIDI AMBACHO HATA MEMBE MWENYEWE ALIKIUNGA SANA MKONO KWENYE KAMPENI ZA URAIS NA SISI WOTE MAGUFULI ALISEMA WAZI KWAMBA TAIFA LIMEOZA MEMBE ALIKUWA NA NAFASI KUBWA KUMKATALIA THEN KWAMBA SIO KWELI TAIFA HALIJAOZA KWA SABABU LABDA MOJA YA SABABU YA MEMBE KUJITOKEZA NOW NA KAULI KALI NI KUJARIBU KUTETEA RECORD YA UTAWALA ALIOKUWA MSHIRIKI WA KARIBU NA RAIS ALIYEPITA BASI ANAKOSEA SANA KWA SABABU TULIMKATAA LOWASAA KWA KUWA ALIKUWA RAFIKI NA MATAJIRI NA WALIOTUAMBIA KWAMBA LOWASSA HAFAI NI PAMOJA NA YEYE MWENYEWE MEMBE SASA LEO KWELI TENA MEMBE ANASIMAMA KUSHAMBULIA KAZI ZA MAGUFULI KWA NIABA YA WAFANYABIASHARA? ….PLEASE MEMBE ATUOMBE RADHI WATANZANIA MILLIONI 50 TULIOMCHAGUA MAGUFULI CAUSE SISI BADO HATUJALALAMIKA KIVILEEE KAMA YEYE MTU MMOJA AMBAYE HAPA ANAKUWA KIGEU GEU NI YEYE MEMBE ALIYESIFIA UAMUZI WA MAGUFULI KUSIMAMISHA SAFARI ZA NJE KWA MAOFISA WA SERIKALI AKASEMA “TULIKUWA TUNAPISHANA JUU KWA JUU KAMA NYUMBANI KUNA MOTO” LEO MWEZI MMOJA NA NUSU LATER MEMBE TENA AMEBADILIKA ANASEMA SAFARI NI LAZIMA? WHY? …..JANA NILIKUWA MSTAARABU KIDOGO NILIDHANI MEMBE ALIPITIWA TU LAKINI KUMSIKIA AKIZUNGUMZA TENA JANA NASEMA HAPANA AGENDA ALIYONAYO MEMBE THIS TIME AROUND SIO YETU WANANCHI NINAANZA KUWA NA WASI WASI LABDA RAIS JK ALIWAPA WATU WENGI VYEO KWA USHAURI WA MEMBE NDIO MAANA SASA ANAUMIA KUONA ALIKUWA ANAMSHAURI VIBAYA RAIS LIKE SIO SIRI MKURUGENZI WA NIDA ALIKUWA NI RAFIKI WA KARIBU SANA WA MEMBE JANA TU IMEDHIRIKA HUENDA AMEFUJA KARIBU TSH. 156 BILLION ZA KODI ZETU KWENYE VITAMBULISHO VYA TAIFA NOW NIAMBIE KIPI CHA AJABU MKURUGENZI WA SHIRIKA LA UMMA AMEPATA WAPI MAPESA YA AJABU MPAKA KUJENGA MRC PALE NYUMA YA SHOPPERS PLAZA MIKOCHEN? …I MEAN KUNA MAMBO MENGINE WANATUFANYA KAMA WATOTO WHY? MEMBE AMEZUNGUMZA KUTETEA WAFANYABIASHARA NA MEDIOCRE LEADERS IT IS WRONG ATUOMBE RADHI WANANCHI! – LE MUTUZ

Rukwa farmers shocked by 'foreign' tomato disease.

 Image result for tomatoes photo
 FARMERS in Nkasi District, Rukwa Region have expressed their fears on the invasion of a dangerous tomato disease known as ‘Tuta Absoluta’, which was for the first time brought into the country in 2014.
 
For the past one year since the tomato disease was reported in the country, it was only found in the three regions of Arusha, Kilimanjaro and Morogoro.
The Southern Highlands zone, which comprises Mbeya, Iringa, Njombe, Ruvuma and Rukwa regions, was free from the disease.
 
According to Nkasi District Agricultural Officer, Henry Sing'ombe, the disease is linked with ‘Tuta Absoluta’—a devastating tomato pest, which originated from South America. 
 
‘Tuta Absoluta’ sucks water from the plant through tomato leaves. The leaves are left with pathogen, which circulate throughout the plant ending up with dried leaves, stem and roots.
 
The official said the disease which was reported to have hit the area in December last year; attacks tomato leaves and thereafter affects the entire growth of the plant.
 
“When studied, we discovered that it’s ‘Tuta Absoluta’ and we started putting in place strategies to arrest the dangerous tomato miner.
 
“The strategies include applying pesticides such as March 500 EC, Actra 25 EC and Buffalo100 EC. We managed to reduce the scale of the disease, but we’ve a lot to do to phase-out the disease,” Sing’ombe said.
 
He added that mixtures of Evisect 50 SP, Escotin 0.15 EC, Covagen 5C and Belt 480 5C, which are very expensive, are also used to contain the disease.
 
“Other strategies include educating farmers on how to tackle the disease; as well as informing them on the need for them to leave farms affected with the disease for a while.”
 
The official said his office has contacted the Agricultural Research Institute - Uyole (ARI-Uyole), so that they come up with long-lasting solutions to the disease.
 
Nkasi District-based farmer Boniface Msafiri said he was afraid that he will not harvest anything in his farm because of the disease.
 
He said that the disease is very challenging and immediate efforts from different players in the agriculture sector are needed.
 
Flora Mwaga, who is a small-scale tomato grower in Sumbawanga District, complaining on the new disease, called upon the government to chip-in and assist them on how to do away with the disease.
 
She also urged extension officers to visit farmers in their farming fields to see how big the scale of the problem is.
 
The Tomato miner ‘Tuta absoluta’ was reported in Tanzania for the first time in August 2014 in Arumeru District, Arusha Region.
 
Recently, ‘Tuta Absoluta’ was considered to be a serious threat to tomato production in the Mediterranean region. The newly imported pest from South America finds the shores of the Mediterranean a perfect new home where it can breed between 10 and 12 generations a year. 
 
Each female can lay 250-300 eggs in her life time.  The pest is crossing boarders and is destroying tomato production both protected and in open fields.

Monday, January 25, 2016

Mama Amuua Mwanae Kwa Kichapo.


Mtoto wa miaka 11, Nchambi Tungu, ameuawa kikatili na mama yake mzazi kwa kuchapwa fimbo kisha kumfunga kamba shingoni na kumning’iniza kwenye tawi la mwembe ili ionekane kuwa amejinyonga mwenyewe.

Inaelezwa kuwa mama wa mtoto huyo, Sado Roketi (26) mkazi wa kitongoji cha Mnyakasi, kijijini Ikuba, wilayani Mlele, mkoa wa Katavi alimuua mwanawe huyo baada ya kukataa kumfulia nguo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, jana alithibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Alisema tukio hilo ni la Januari 23, mwaka huu saa moja jioni katika Kitongoji cha Mnyakasi. Alisema siku ya tukio mtuhumiwa alimpatia mwanawe huyo nguo amfulie lakini mtoto huyo alikataa kuzifua akaendelea kucheza na wenzake.

“Ndipo mama huyo kwa hasira alipoamua kuchukua fimbo na kuanza kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake na kumsababishia kifo, aliubeba mwili na kuutundika kwenye matawi ya mti wa mwembe baada ya kumfunga kamba shingoni na kumwacha akining`inia ili ionekane alijinyonga mwenyewe,” alieleza Kidavashari .

Alisema mtuhumiwa anashikiliwa na Polisi na atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.

Friday, January 22, 2016

HII NDIO SHUGHULI YA WANCHI WA MKOA WA SONGWE NA MAZINGIRA.


WanaTAJATI pia walipata fursa ya kushiriki upandaji wa miti kuzunguka eneo la Hospitali ambapo miti zaidi ya 50 ilipandwa


Mbali na kupanda miti pia walifanya usafi katika mazingira yanayoizunguka Hospitali ya Wilaya ya Chunya

TAJATI wakishiriki ujenzi wa daraja kubwa lililojengwa kwa nguvu za wananchi wa Kijiji cha Igangwe kata ya Mtanila Wilaya ya Chunya linaloviunganisha vitongoji vya Shauri Moyo na Mtukula

Mwenyekiti wa TAJATI Ulimboka Mwakilili akishirikiana na Mwenyekiti wa Igangwe Amcos kuzindua zoezi la upandaji wa miti katika Shamba la Chama cha Msingi cha Igangwe ambapo miti zaidi ya 1000 ilipandwa

Wakulima wa Igangwe amcos wakishirikiana na Wanachama wa TAJATI katika upandaji wa miti

Makamu Mwenyekiti wa TAJATI, Christopher Nyenyembe akikagua timu za mpira wa miguu kabla ya kuanza kwa mtanange katika kuadhimisha mapinduzi ya Zanzibar


Mtunza Hazina wa TAJATI, Brandy Nelson akimkabidhi zawadi nahodha wa timu ya msindi wa Kwanza katika mechi maalum ya kuenzi mapinduzi ya Zanzibar

Katibu Mkuu wa TAJATI, Venance Matinya, akimkabidhi zawadi ya mpira wa miguu nahodha kwa niaba ya timu yake baada ya kuibuka kidedea katika shindano maalum la kuenzi mapinduzi ya Zanzibar lililofanyika Lupa wilayani Chunya

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Sophia Kumbuli akiwa katika kikao cha majumuisho ya ziara ya waandishi wa Habari za Utalii na Uwekezaji (TAJATI).

Makamu Mwenyekiti wa TAJATI akiagana na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
 
 
BAADHI ya Wanachama wa Chama  cha Waandishi wa habari za Utalii na Uwekezaji Tanzania(TAJATI) walifanya ziara ya siku tatu katika Wilaya ya Chunya na kushiriki shughuli mbali mbali za kijamii na kihabari.
 
Waandishi hao walifanya ziara hiyo jumatatu na kukamilisha jumatano ya wiki hili ambapo wakiwa Wilayani Chunya walipokea taarifa ya hali ya utalii ya Wilaya ya Chunya na kushiki shughuli za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea wagonjwa katika Hospitali ya Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya.
 
Akizungumza katika majumuisho ya Ziara hiyo iliyojumuisha waandishi 12, mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Chunya, Sophia Kumbuli, Mwenyekiti wa TAJATI, Ulimboka Mwakilili alisema katika ziara hiyo iliyokuwa na mafanikio imepokelewa vizuri na wananchi.
 
Alisema siku ya kwanza waandishi waliweza kutembelea wagonjwa na kutoa zawadi kidogo ikiwemo sabuni za kufulia na vinywaji aina ya Grandmalt kwa ajili ya kuongeza nguvu sambamba na usafi wa mazingira ulioenda sambamba na uzinduzi wa kupanda miti ambapo miti zaidi ya 50 ilipandwa kati ya 560 inayotarajiwa kupandwa na Hospitali hiyo.
 
Aliongeza kuwa siku ya pili waandishi hao walishiriki katika ujenzi wa daraja la Mto Lupa katika Mto kijiji cha Igangwe linalounganisha Kijiji hicho na Vitongoji wa Shauri Moyo na Mtukula lenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni Mbili.
 
Aliongeza kuwa baada ya kushiriki ujenzi wa daraja hilo waandishi hao pia walijumuika na wakulima wa Chama cha Msingi cha Igangwe Amcos katika zoezi la upandaji wa miti ambapo zaidi ya miti laki moja ilipandwa ikiwa ni kutekeleza utunzaji wa mazingira na kampeni ya kata mti  panda miti.
 
Zoezi hilo la upandaji miti limetokana na wakulima wa Tumbaku kutumia miti kwa kiasi kikubwa wakati wa kuandaa zao la Tumbaku hadi mavuno jambo lililopelekea uongozi wa Amcos kuweka sheria na kanuni kwa kila mkulima kuhakikisha anapanda miti 500 katika shamba la Chama cha msingi na 25 shambani kwake.
 
Mwakilili alisema mbali na kushiriki shughuli hizo pia waandishi walizungumza na wananchi kuhusu changamoto zinazowakabili ambapo mambo mengi yalibainishwa ikiwemo ndoa za utotoni, mimba mashuleni na upungufu wa wahudumu wa afya katika kituo cha Afya Mtanila ambacho kina watumishi wanne tu.
 
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Sophia Kumbuli mbali na kuwapongeza WanaTAJATI  kwa ziara yao pamoja na shughuli zingine za kimaendeleo na kijamii aliahidi kuyafanyia kazi mapungufu yaliyobainishwa.
 
Kuhusu ndoa za utotoni Mkurugenzi alisema atawasiliana na Kamati ya Ulinzi na uasalama ya Wilaya ili kuanza utekelezaji wa kuwasaka wanaume wanaooa mabinti wadogo na kuwakatika katika masomo yao.
 
Alisema suala la afya kutokuwa na watumishi wa kutosha alisemahilo ni tatizo la Wilaya nzima ingawa Serikali inatarajia kutangaza nafasi za kuajiri hivyo tatizo hilo linaweza kupungua kwa kiasi Fulani.
 
“Niwapongeze kwa juhudi zenu na ninawaahidi kuyafanyia kazi mambo yote mliyoyabaini mkiwa Wilayani Chunya hususani suala la kuozesha watoto wadogo hili limenisikitisha mno na sitalifumbia macho nitatoa taarifa kwa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ili wahusika wasakwe mara moja huu ni ukatili wa kijinsia” alisisitiza Mkurugenzi.

Thursday, January 21, 2016

NECTA YATANGAZA MATOKEO YA DARASA LA IV

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya mitihani ya kujipima ya darasa la nne huku matokeo hayo yakionyesha wanafunzi wengi wamefeli katika somo la Kiingereza kwa asilimia 65.67 katika mitihani hiyo iliyofanyika mwishoni 2015.

Akitangaza matokeo hayo leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza hilo Dkt. Charles Msonde amesema juhudi za makusudi zinahitajika katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzia ili kuboresha kiwango cha ufaulu.

Jumla ya wanafunzi 869,057 kati ya wanafunzi 977,886 sawa na asilimia 88.87 waliofanya upimaji wamepata alama katika madaraja ya A,B,C,na D. Wanafunzi 108,829 sawa na asilimia11.13 wamepata alama za ufaulu usioridhisha.
Aidha wanafunzi wamefanya vizuri zaidi katika somo la Sayansi kwa asilimia 89.44, na baraza limewataka walimu kuweka mkazo zaidi kwa wanafunzi waliofanya vibaya ili wafanye vizuri.

NATIONAL EXAMINATIONS COUNCIL OF TANZANIA

SFNA-2015 ASSESSMENT RESULTS